MGOGORO WA ARDHI KWISHA, UJENZI WA KITUO CHA AFYA KIMANGA KUANZA – Dar es salaam News

Na Dar es Salaam News

Wakazi wa Kimanga na Segerea katika Jimbo la Segerea wana sababu ya kufurahia baada ya Mbunge wao, Bonnah Kamoli, kutangaza kwamba mgogoro wa ardhi uliokuwa ukikwamisha ujenzi wa Kituo cha Afya Kimanga umemalizika. Ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kuanza wakati wowote.

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mgogoro huo wanajipanga kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho, hivyo wakazi hao wasiwe na wasiwasi. Kwa kukumbusha tu, Mbunge Bonnah katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro uliokuwepo aliamua kumpeleka Waziri wa TAMISEMI ambaye alitoa maelekezo ya kufanywa na Halmashauri ya Jiji. Maelekezo yametekelezwa na tayari fidia ya Sh. 33.9 milioni imelipwa kwa aliyekuwa amefanya maendeleo eneo hilo, yaani Muungano Culture Troupe.

Muda wowote kuanzia sasa eneo hilo litatumika kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Kimanga,” alisema Mbunge Kamoli.

Aidha, Mbunge wa Jimbo la Segerea amewaambia wananchi wa Mtaa wa Twiga – Kimanga kuwa tayari serikali imetoa fedha kiasi cha Sh. milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa kivuko kinachotoka Twiga kwenda Makubuli ambacho kilikuwa kero sana kwao. Amesisitiza kuwa fedha ipo kwenye akaunti ya kata na kwa sasa harakati za kumtafuta Mkandarasi zinaendelea.

Sambamba na hayo, Bonnah anafahamu adha kubwa wanayoipata wananchi wa Kimanga kutokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara. Amefafanua tayari fedha ya dharura imekwishapatikana kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Tabata Bima – Darajani – Mawenzi – Kimanga – Majichumvi na muda wowote ukarabati utaanza.

Pia, tayari manunuzi yamekwishafanyika kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami, mitaro, vivuko na taa za mwanga wa usiku katika barabara za Mwananchi – Savannah, Barakuda – Chang’ombe – Mazda na BC.

Pamoja na hayo, Bonnah amesema anatambua namna wana Kimanga walivyokuwa wavumilivu na anawahakikishia kuwa sasa changamoto walizokuwa nazo hasa upande wa miundombinu ya Afya na barabara zinaenda kutatuliwa.

Faida za Kituo cha Afya Kimanga kwa Wakazi na Taifa

Kuboresha Huduma za Afya

Kituo cha Afya Kimanga kitarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa Kimanga na Segerea, kupunguza umbali wa kusafiri kwa huduma za matibabu.

Kupunguza Msongamano

Kituo hiki kipya kitapunguza msongamano katika vituo vingine vya afya vilivyoko jirani, hivyo kuboresha huduma kwa wote.

Ajira kwa Wakazi wa Kimanga

Ujenzi na uendeshaji wa kituo cha afya kutaongeza fursa za ajira kwa wakazi wa eneo hilo, ikiwemo nafasi za ujenzi, uuguzi, na usimamizi.

Maendeleo ya Miundombinu

Mbunge Kamoli pia alitangaza kuwa serikali imetoa Sh. milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa kivuko kutoka Twiga kwenda Makubuli, na fedha za dharura kwa ajili ya ukarabati wa barabara ya Tabata Bima – Darajani – Mawenzi – Kimanga – Majichumvi zimepatikana.

Ukarabati wa Barabara na Miundombinu

Mbunge ameeleza kuwa manunuzi yamefanyika kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami, mitaro, vivuko na taa za mwanga wa usiku katika barabara za Mwananchi – Savannah, Barakuda – Chang’ombe – Mazda, na BC.

Mchango kwa Taifa

Ujenzi wa kituo cha afya Kimanga ni sehemu ya jitihada za serikali za kuboresha huduma za afya nchini. Kwa kupunguza mzigo kwenye hospitali kubwa na kuhakikisha huduma zinapatikana kwa urahisi, taifa litaweza kuhudumia wananchi wake kwa ufanisi zaidi, kuimarisha afya ya jamii na kuongeza tija katika sekta nyinginezo.

Kwa wakazi wa Kimanga, ujenzi huu ni ahueni kubwa na hatua muhimu kuelekea maendeleo ya afya na miundombinu. Mbunge Kamoli ameahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa serikali kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati na kwa viwango vya juu.

Picha kwa hisani ya Mtezamedia

Kwa habari zaidi na matukio yanayoendelea, endelea kufuatilia daressalaamnews.co.tz, share na uwapendao kwa habari hizi muhimu.

Share.

1 Comment

  1. Pingback: KUMBILAMOTO AGAWA BURE BIMA YA AFYA KWA WATU 114 VINGUNGUTI – Dar es salaam News

Leave A Reply

Exit mobile version