- Utangulizi
- Maelezo ya jumla kuhusu Taasisi ya Kumbilamoto Foundation
- Uzinduzi wa Bima ya Afya
- Tukio la uzinduzi wa bima ya afya kwa watu 114 wa Vingunguti
- Kadi za bima zilizotolewa kwa kaya 19
- Faida za Bima ya Afya
- Umuhimu wa bima ya afya kwa wananchi
- Manufaa ya bima ya afya kufikia gharama za matibabu
- Mchango wa Taasisi ya Kumbilamoto Foundation
- Historia na malengo ya Taasisi ya Kumbilamoto Foundation
- Huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi
- Sifa kwa Viongozi na Wadau
- Mafanikio ya serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan
- Pongezi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Segerea
- Matokeo na Thamani ya Kadi za Bima
- Thamani ya kadi za bima zilizotolewa kwa wananchi
- Wanufaika na mitaa iliyopokea kadi za bima
- Huduma za Zahanati ya Vingunguti
- Huduma zinazotolewa na Zahanati ya Vingunguti
- Upatikanaji wa huduma za afya saa 24
- Hitimisho
- Matumaini na matarajio ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Vingunguti
Na Dar es salaam News
TAASISI ya Kumbilamoto Foundation imetoa bima ya afya kwa Watu 114 bure wa kata ya Vingunguti wilayani Ilala mkoa Dar es Salaam, kwa ajili ya kusaidia wananchi huduma za matibabu katika hospitali na vituo vya afya..
Uzinduzi huo wa kugawa Bima ya afya ulianzia Zahanati ya Vingunguti ulinzinduliwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Said Sidde ambapo aliwapa kadi za Bima ya afya kaya 19 sawa na Wananchi 114 wa mitaa sita ya Vingunguti.
Mwenyekiti WEN wa CCM Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam Said akiizungumza mara baada kuzindua ugawaji wa Bima ya Afya Bure kwa watu 114,amesema mtaji wa mwanadamu ni afya hivyo Taasisiya Kumbilamoto Foundation imejali afya za wananchi wa Vingunguti ni jambo la kumshukuru Mwenyenzi Mungu kila wakati.
“Mwenyekiti Side alisema kadi ya Bima ya afya ni muhimu unaweza ukaitumia kupimia matibabu mpaka ya Sh 700,000 au milioni kwa ajii ya vipimo peke yake hivyo wananchi wana umuhimu wa kukata bima ya afya tunaishukuru taasisi ya Kumbilamoto Foundation kwa kujali wananchi wa kata ya Vingunguti alisema Sidde
Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbilamoto Foundation Omary Kumbilamoto alisema Taasisi ya Kumbilamoto Foundation imeanzishwa mwaka 2021 na kusajiliwa kwake mwaka 2022 inatoa huduma za kijamii sehemu zote ikiwemo kuchimba visima na kusaidia makundi maalum wakiwemo Wazee Wajane na Vijana ili kuondoa changamoto zao
Amesema miaka mitatu ya Dkt.Samia Suluhu Hassan nchi yetu imepata mambo makubwa ya maendeleo ambapo alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Jamary Mrisho Satura na Mbunge wa Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli kwa kufanya mambo makubwa ya maendeleo Kata ya Vingunguti na jimbo la Segerea kwa ujumla .
Katibu wa Taasisi ya Kumbilamoto Foundation Alex Buberwa alisema wananchi 114, wamepewa kadi bure zenye thamani ya shilingi millioni 2.8 alisema taasisi hiyo imejikita zaidi kusaidia jamii leo wametoa mitaa sita ya Vingunguti ikiwemo Mtakuja,Majengo Mtambani,Butiama,Miembeni na Kombo kwa lengo la wananchi wa maeneo hayo waweze kuzitumia kadi hizo katika huduma ya afya.
Faida za Bima kwa Wananchi
1. Upatikanaji wa Huduma za Afya Bila Kizuizi cha Gharama
– Bima ya afya inawawezesha wananchi kupata matibabu bila kuwa na wasiwasi wa gharama kubwa zinazohusiana na huduma za afya. Hii inamaanisha kuwa matibabu yoyote muhimu yanaweza kupatikana mara moja bila kucheleweshwa kutokana na ukosefu wa fedha.
2. Gharama za Matibabu Zilizo na Mpaka
– Kadi za bima ya afya zinaweza kufidia gharama za matibabu hadi kiwango fulani, kwa mfano hadi TZS 700,000 au hata zaidi kwa ajili ya vipimo peke yake. Hii inapunguza mzigo wa kifedha kwa familia na inahakikisha kuwa wanapata huduma bora za afya.
3. Ulinzi Dhidi ya Dhiki ya Kifedha
– Kuwa na bima ya afya husaidia kuepuka matatizo ya kifedha yanayoweza kutokea kutokana na gharama za ghafla za matibabu. Hii ni muhimu sana kwa familia zenye kipato cha chini na cha kati.
4. Upatikanaji wa Huduma Bora za Afya
– Bima ya afya inawapa wananchi nafasi ya kupata huduma bora za afya katika hospitali na vituo vya afya vilivyoidhinishwa. Hii inajumuisha huduma za vipimo, matibabu, na upasuaji, ambazo zinaweza kuwa ghali bila bima.
5. Kuboresha Afya na Ustawi wa Jamii
– Wakati wananchi wanapokuwa na uhakika wa kupata huduma za afya, wanakuwa na uwezekano mdogo wa kuacha matibabu muhimu. Hii inaboresha afya ya jumla ya jamii na kuongeza ustawi wa wananchi.
6. Uhamasishaji wa Matumizi ya Huduma za Kinga
– Bima ya afya pia inahamasisha wananchi kutumia huduma za kinga kama vile chanjo na vipimo vya kawaida. Hii husaidia kugundua na kutibu magonjwa katika hatua za awali kabla hayajawa makubwa.
7. Kuongeza Ufanisi na Ubora wa Huduma za Afya
– Kwa kuwa bima ya afya inahusisha hospitali na vituo vya afya vilivyoidhinishwa, inachangia katika kuboresha ubora na ufanisi wa huduma zinazotolewa. Taasisi za afya zinalazimika kuzingatia viwango vya juu vya huduma ili kukidhi mahitaji ya watoa bima.
8. Kuimarisha Usalama wa Afya
– Bima ya afya inatoa usalama wa kiafya kwa familia, kuhakikisha kuwa kila mwanachama wa familia anaweza kupata matibabu bila kuchelewa. Hii ni muhimu hasa kwa watoto, wazee, na watu wenye magonjwa sugu.
Kwa jumla, bima ya afya ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha afya bora na ustawi wa wananchi, huku ikipunguza mzigo wa kifedha unaohusiana na gharama za matibabu.
Wakati huo huo Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Vingunguti Isack Makundi amesema kwa sasa Zahanati ya Vingunguti inatoa huduma saa 24 na baadhi ya huduma hizo Kinywa na Meno ,Tiba ya mionzi (Utrasound )Wodi ya Wazazi kwa ajili ya kuzalisha kiliniki ya Baba Mama na Mtoto,TB na Ukoma ,Upasuaji mdogo ,matibabu ya wagonjwa wa nje .