Utangulizi
- Maelezo ya jumla kuhusu Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT)
Agizo la Vikao Kazi
- Makatibu wa Umoja kuandaa vikao kazi
- Umuhimu wa kufuata kanuni za Jumuiya
Kuongeza Wanachama
- Mkakati wa kuongeza wanachama wapya
- Usajili wa wanachama kwa kutumia kadi za kisasa za ELECTRONIC
Mabadiliko ya Viongozi
- Kuwafuta kazi viongozi wasioshiriki vikao
- Uchaguzi wa viongozi wapya
Uhamasishaji wa Uchaguzi
- Wanawake kuchukua fomu za uchaguzi wa Serikali za mitaa 2024
- Kujiandikisha katika Daftari la Makazi na Daftari la mpiga kura
Ziara ya UWT Mkoa
- Madhumuni ya ziara ya UWT mkoa
- Tathmini ya uhai wa Jumuiya na uingizaji wanachama ngazi ya matawi
Mafunzo na Maazimio
- Mafunzo yaliyopatikana kutoka ziara ya UWT Kimanga
- Maazimio ya kufanya kazi kwa weledi kuelekea uchaguzi
Hitimisho
- Matumaini na matarajio ya Jumuiya kwa siku za usoni
Na Dar es Salaam news
JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT) Mkoa wa Dar es Salaam imewaagiza Makatibu wa Umoja huo ngazi ya kata na matawi kufanya vikao kazi kulingana na kanuni zilizowekwa na Jumuiya hiyo.
Katibu wa UWT Mkoa Dar es Salaam Asha Stambuli ameyasema hayo wakati wa ziara yake na Kamati ya Utekelezaji UWT Mkoa Jimbo la segerea ambapo amewaomba Makatibu hao kufanya kazi za jumuiya, vikao na kusoma kanuni kwa ajili ya kuongoza jumuiya vizuri.
Amefafanua ili Jumuiya iweze kusonga mbele ni lazima viongozi wake wafanye kazi na kufuata Kanuni ya Jumuiya inavyoelekeza mambo mbali mbali ikiwemo kufanya vikao .
Ameongeza kwamba ili Jumuiya iweze kusonga mbele lazima iwe na mtaji wa Wanachama wengi hivyo aliwataka kila kiongozi wa Kamati ya Utekelezaji kuleta wanachama wapya na kuwasajili katika mfumo wa kadi za kisasa za ELECTONIC.
Wakati huo huo aliwataka UWT Jimbo la segerea na Kimanga viongozi waliochaguliwa na kushindwa kushiriki vikao na kufanya kazi waondolewe wachaguliwe Wengine kuziba nafasi zilizopo wazi.
Katika hatua nyingine Katibu wa Mkoa wa UWT aliwamasisha wanawake kuchukua fomu ya uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa ajili ya kugombea mwaka huu 2024.
Pia alihamasisha Kushiriki kujiandikisha katika Daftari la Makazi na Daftari la mpiga kura waweze kupata haki ya msingi ya kupiga kura katika uchaguzi wa Serikali za mitaa .
Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Ilala Mariam Bakari alisema dhumuni la ziara ya UWT mkoa kuangalia uhai wa jumuiya na uingizaji wanachama ngazi ya matawi ambapo pia aliwataka UWT Kimanga kuongeza wanachama wapya na kufanya vikao kila mwezi.
Awali Mwenyekiti wa UWT Kimanga Dkt.Marysia Tukai amesema katika ziara hiyo UWT Kimanga wamejifunza mambo mengi na wamepata chakula ya ubongo hivyo watafanya mambo makubwa kwani imekuwa chachu ya kuongeza kufanya kazi kwa weledi kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa.